- Nami nasema haya;
Kwa waamini; kifo si mwisho wa yote...bali ni daraja katika kuyaendea maisha ya uzima wa milele!
Ni daraja kutoka katika maisha haya yanayogubikwa na simanzi - mateso na kuingia katika maisha ya uzima wa milele na kwamba; kifo si mwisho wa yote katika hija ya mwanadamu, ki maumbile watu hawataweza kumwona tena Asifiwe, wala kuonja upendo na ukarimu wake. Kifo ilivyo kawaida kinaleta masikitiko, majonzi na huzuni na wakati mwingine kinaambatana na manung'uniko mbalimbali. Ki msingi hakuna sababu ya kulalamika kutokana na kifo, kwani ukiamini katika fumbo la ufufuko na maisha ya uzima wa milele. Jambo la msingi sana ni kuendelea kumwombea Asifiwe, ili Mwenyezi Mungu apende kumweka miongoni mwa wateule wake mbinguni, na kama bado anayo mapungufu kama binadamu basi aweze kutakaswa....ili hatima yake aonje pendo na huruma ya Mungu aliyoitumainia katika maisha yake.
Maisha ya duniani yanapita: yana furaha, utukufu na mahangaiko yake....changamoto kwetu sisi sote kuchuchumilia utukufu wa mbinguni na maisha yenye uzima wa milele.
- Mwenyezi Mungu tunakuomba kwa huruma yako uendelee kumlaza Asifiwe mahali pema peponi.....Amina!
No comments:
Post a Comment