Thursday, December 15, 2011

AMA KWA HAKIKA HII NDIO TANZANIA....TUNAYOSEMA;.....

.....Ina Amani na kuheshimu haki za raia wake, hebu angalia hawa Askari wakimsurubu Kijana huyu ambaye si kibaka bali ni raia mwema tu! lakini kwasababu wao wanazozijua wanampa kosa la kuwakimbia na Pikipiki wakati wakimsimamisha barabarani, lakini si kweli....Kijana huyu ni muuza maji na juice kwenye kituo cha basi, hata hilo Pikipiki lenyewe halijui.
Lakini ndio hivyo wameshaamua kutoa kichapo hicho, sasa tujiulize mimi na wewe kuna haki hapa kweli? na hiyo Amani wanayoihubiri kila kukicha iko wapi? Inasikitisha sana kuona Mtanzania akinyanyaswa kwa kosa ambalo hakufanya bali amefananishwa tu! na mtu mwingine. Ni wangapi wameonewa, wamenyang'anywa mali zao na wana usalama wa Bongo?
Binafsi sikufurahishwa kabisa na nimeumizwa sana na kitendo hiki. Tanzania hakuna Amani....bali kuna ukimya tu! Hao Polisi hawajui kabisa mipaka ya kazi yao, wanadhani kupiga raia ni kazi yao.

- Mimi binafsi ninachojua Polisi anatakiwa kulinda usalama wa raia na sio kupiga raia....hata kama kweli kafanya kosa, walipaswa kumkamata na kumpeleka Kituoni na kumuhoji wajue kisa cha kuwakimbia na kama ni yeye ama siye! sio kwa kumfananisha tu.
Kwakweli Watanzania inabidi tufike sehemu tuseme sasa basi, tukiona wenzetu wananyanyaswa na hawa Polisi....tuchukue hatua za kuingilia na kuwatetea wenzetu.
Huwezi jua lini yatakukuta na wewe ukafananishwa tu na jambazi sugu, wakaishia kukupiga risasi bila ya kupewa nafasi ya kujieleza na kujitetea.

No comments:

WATEMBELEAJI