Wednesday, December 14, 2011

HAYA MAMBO YAPO SANA SIKU HIZI BONGO...ILA MI SIMO!

Jamaa kajisahau na mlio wake wa simu...ambao sio mahali pake kabisa...sasa kilichoendelea hapo mimi sikuwepo! Maana mmmmhhhh.....!!!!!! Jaribu kuimajini mwenyewe ilikuwaje!



Haya mambo nimeyaona sana Bongo ya mtu kujichanganya unakuta kanogewa tu na hizi nyimbo...awe wa dini yoyote ile. Ila mi hapa sipo kabisaaaa....!!!! Sitaki ugomvi na mtu wala kumchongea mtu. Maana mambo kama haya ya nyimbo hizi kwa Tanzania yetu yapo kila kona siku hizi...mpaka kwenye Baa utakuta zinapigwa kwa sana nyimbo hizi maarufu kama huu wa Nibebe, wa Rozi Muhando. Sasa hapa Jamaa wenzake sijui ilikuwaje...maana mmmhhh!!!!






- Ila nyimbo hizi zinazo shika kasi sana Tanzania a.k.a maarufu....huwa zina utamu wake, utakuta kila mtu anazijua...siku moja nilikutana na Kibibi kizee kimoja kinaimba kwa raha zake, tena kilikuwa tungi sana (Kimelewa), nilicheka mpaka basi. Mpaka leo hii nakumbuka sana!

2 comments:

WATEMBELEAJI