Monday, December 5, 2011

KWA RAHA ZAKE.....KAZI INAENDELEA TU! HAPA HAMNA HATARI.

Tungelikuwa tunazingatia usalama makazini kwetu.....Tanzania tungelikuwa mbali sana ki maendeleo, maana tusingepoteza watu kwa ajali zisizo na msingi....ovyo ovyo tu, kila kukicha watu wanakufa bila ya uangalifu. Angalia hapa huyu fundi wa Umeme wa Tanesco alivyo makini kwa usalama wa maisha yake na kazi yake. Je tunajifunza nini katika miaka hamsini ya Uhuru wa Bendera? Au ni uhuru wa nchi tu! uhuru wetu wa mawazo vipi?

- Kila lakheri nyingi Tanzania yangu/yetu.....na tuzidi kudumisha mawazo mema na fikra njema!
Mwenyezi Mungu Ibariki Tanzania na watu wake wote....Ibariki Afrika na Dunia nzima!

No comments:

WATEMBELEAJI