Monday, December 5, 2011

KWAHERI RAFIKI MR.EBBO.....PUMZIKA KWA AMANI.

Msalaba wa Jeneza la Abel Motika a.k.a Mr.Ebbo, ni ishara ya kuonyesha kuwa apumzike kwa amani...msalaba ndio ukombozi wake katika nyumba yake ya milele! Hii picha ilikuwa inaonyesha mwili mzima wa Mr.Ebbo, lakini mimi sijapenda sana....maana sio vizuri sana kuonyesha mwili wa Marehemu.

Baadhi ya Ndugu, Jamaa na Majirani....wakiuaga mwili wa Marehemu Mr.Ebbo, leo hii huko Arusha.



Mke wa Marehemu Mr.Ebbo kulia, akiwa ameshikiliwa mara baada ya kuuaga mwili wa mumewe.





Wazizi wa Marehemu kutoka kulia ni; Baba yake na Mama yake.

Katika mazishi yake Mr.Ebbo...leo hii huko Mjini Arusha - Tanzania.







1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Mungu alitoa na mungu amechukua. Poleni wafiwa, ndugu, jamaa na marafiki. Ni msiba wa wote...jamani kumbe alikuwa hata 40 hajafikisha. Ustarehe kwa amani tutakukumbuka daima.

WATEMBELEAJI