Watanzania wote leo tunafuraha sana ya kusherekea sherehe hii kubwa ya miaka 50 ya Uhuru wetu toka tumejikomboa kwa mkoloni. Siku ya leo hatuna budi kufurahi sana na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa mema mengi anayotukirimia sisi Watanzania, hasa kabisa swala kubwa sana la amani tuliyonayo, nami nasema hivi;
- Asante sana Mwenyezi Mungu, tunakushukuru sana tena sana tu! kwa mema yako uliyotujalia sisi wanao Watanzania kwa kufikisha miaka 50 ya Uhuru wetu......umoja na mshikamano hizi ndizo nguzo zetu Watanzania. Na bado tuna amani hapa kwetu Tanzania ni jambo la kujivunia sana na kukushukuru sana wewe Baba yetu, twasema; asante sana Baba Mungu. Leo Tanzania yetu ni mfano wa kuingwa kwa mataifa mengi katika dunia hii hasa kwa Afrika yetu hii. Twakusihi ee Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, uzidi kutuangalia; amani na umoja vipate kudumu daima hapa kwetu Tanzania.
Watanzania wote hatuna budi kumshukuru sana Mwenyezi Mungu aliyetujalia hivi......kutujalia imani hii siku za kale na siku hizi, nasi tumwombe neema kubwa ya kudumu siku zote!
Tanzania leo shangwe.....Tanzania leo furaha kubwa; tumejaliwa imani hii muda wa miaka 50, basi, tufurahi na kushukuru sana. Furaha ndio fahari yetu hapa nchini...basi tuzidi kufurahi daima. Tanzania leo bado yahitaji wafanyakazi wengi, kwani kazi ni nyingi katika kujenga Taifa letu ili liweze kuimarika zaidi na zaidi.
- Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania na watu wake wote.....Mungu ibariki Afrika na dunia kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment