Thursday, December 8, 2011

PUMZIKA KWA AMANI BABU BLEZI CHIBIRITI.

Leo jioni yalikuwa mazishi ya Babu yangu mpendwa Mzee Blezi Chibiriti, huko Kijijini Chibumagwa - Manyoni. Nimewasiliana na wanyumbani wamesema; mambo yote ya mazishi yameenda vizuri, ila mvua ilinyesha kubwa sana baada ya mazishi yake kuisha, naamini na kufurahi kuwa ni ishara nzuri. Waliweza kupata ujumbe wangu nilioutuma kwa njia ya barua pepe ili waweze kuusoma katika maishi hayo ili nami niungane nao katika mazishi hayo hata kama nipo mbali na huko nyumbani. Watu walihudhulia wengi, watoto wake wote 8 walikuwepo, wajukuu kwa wingi mpaka Vitukuu. Ninawashukuru wote Wadau wangu kwa mchango wenu wa sala zenu katika kuwombea Babu yangu, ili asamehewe mapungufu yake aliyokuwa nayo hapa Duniani, na apate kuonja Pendo la Mwenyezi Mungu na kupumzika kwa amani.

- Pumzika kwa amani Mpendwa Babu.


3 comments:

Rachel Siwa said...

Pole sana kaka Chibiriti na Familia yote ya Chibiriti,Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa!!!!!!

Baraka Chibiriti said...

Asante sana Dada a.k.a Swahili na Waswahili, kweli kabisa Bwana ametoa na Bwana ametwaa!!! yote ni mapenzi yake tu!

Asante sana Dada.

Yasinta Ngonyani said...

Babu Blezi pumzika kwa amani na tunaomba utuombee nasi kwani siku moja tutakutana.

WATEMBELEAJI