Tuesday, December 6, 2011

LEO NILIKUWA KWENYE UPAKIAJI WA KONTENA YA TANZANIA.

AMICO SOLE PER TANZANIA........AMICO SOLE KWAAJILI YA TANZANIA. Hiki ni kiwanda-Kampuni; Amico sole (Rafiki wa Jua) kwaajili ya Sola Power a.k.a Umeme wa jua. Kiwanda pia kinajishughulisha na mambo ya misaada mbalimbali kwa Afrika yetu. Tripu hii wameamua kuiona Tanzania kwa kutuma vifaa mbalimbali vya mambo ya Umeme wa Jua na nyumba za kutengeneza kwa haraka...nyumba ambayo inakuwa na kila kitu inaunganishwa kwa siku 2 tu! Vifaa hivi vitapelekwa Misheni kwaajili ya msaada wa hawa Jamaa Amico Sole. Niliitwa leo ili kushuhudia na kuwasaidia kupakia Kontena hili na jingine lilikuwa likielekea Nchini Uganda. Nafurahi sana kwa wito huu na msaada huu kwa nchi yetu. Leo nilishinda huko kwa kazi mbalimbali hususani upakiaji wa Kontena hili, niliitikia wito huu kwa moyo wangu wote, na wao wanapenda sana nifanyenao kazi huko Tanzania....bado nafikiria.











Godaoni (Ghala) la Amico Sole....la kuhifadhia vyombo mbalimbali vya mambo ya Umeme.






No comments:

WATEMBELEAJI