Tuesday, December 6, 2011

MAELFU WAMZIKA MR.EBBO....HAPO JANA MJINI ARUSHA!



Maelfu ya Wakazi wa Mji wa Arusha, jana waliungana na Wanafamilia wa Msanii maarufu Mr.Ebbo, katika Misa maalum ya kuuombea mwili wa marehemu Mr.Ebbo. Na baadae katika maziko yaliyofanyika Mjini humo.

Miongoni mwa Viongozi walioshiriki mazishi ni pamoja na; Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh.Goodluck Ole Medeye....ambaye ni Mbunge wa Arumeru Mashariki, pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Dr.Badilda Buriani.....na Wasanii mbalimbali wa Muziki nchini.



Wazazi wa Mr.Ebbo wakiwa na Mbunge wa Zamani na Waziri wa Mazingira Dr.Batilda Buriani.






Watoto watatu wa Marehemu Mr.Ebbo....wakiwa na majonzi makubwa baada ya kifo cha Baba yao Mr.Ebbo.







Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi, Mh.Goodluck Ole Medeye, kulia akimfariji mzazi wa marehemu Mr.Ebbo, Mzee Loshilaa Motika...katika Ibada ya mazishi, nyumbani kwake Moshono - Arusha.









Kaka Mkubwa wa Marehemu Mr.Ebbo, Olais Motika, kushoto na mdogo wake wa mwisho Jackson Motika...wakiwa na majonzi katika Ibada ya mazishi ya ndugu yao mpendwa Mr.Ebbo.

























Maelfu ya Wakazi wa Mjini Arusha...wakiwa katika foleni ya kwenda kutoa heshima za mwisho kwenye mwili wa marehemu Mr.Ebbo.














No comments:

WATEMBELEAJI