MAMBO YA ULANZI......NDANI YA MKOA WA IRINGA.
Ulanzi - Pombe maarufu sana Mkoani Iringa - Tanzania, hapa ikisafirishwa kwenda kunyweka.....kando kando ya barabara kuu ya Iringa - Mbeya. Hawa jamaa mara nyingi nimewaona wakiendesha baiskeli huku wakiwa na mipira wakinyonya (wakinywa) huku safari ikiendelea, mipira hiyo ionekanayo hapo nyuma ya madumu.....barabara hii huwa wabishi sana kupisha magari, na mara nyingi hugongwa! Sijui kwanini watu tunakuwa wagumu na hatuelewi thamani ya maisha....huwa sielewi kabisa!
2 comments:
Je hiyo mipira wanayonyonyea inasafishwa?...Ingekuwa vizuri kama kungekuwa na barabara kwa ajili ya baiskeli tu. Hakika kungekuwa na unafuu sana kwa wote.
Kweli kabisa Dada Yasinta....na wasiwasi sana na hiyo mipira kama inaoshwa kweli.
Post a Comment