Kipindi cha majilio ni wakati wa kusikiliza kwa makini sauti ya Mungu, iliyo jangwani.
Waumini tujiandae kwa ujio wa Kristu, kwa kusikiliza kwa makini sauti hii nzuri ya Mungu iliyo jangwani...kupitia usomaji wa maandiko matakatifu.
Furahini katika Bwana siku zote; tena nasema furahini......Bwana yu karibu!
Waambieni walio na moyo wa hofu....jipeni moyo msiogope; tazama...Mungu wetu atakuja na kutuokoa.
Ee Bwana utujalie huruma yako....utuondolee dhambi zetu; na neema zako hizi zituweke tayari kuadhimisha sikukuu zijazo.
2 comments:
Hakika ni maneno mazuri ..Amina
Asante sana Dada Yasinta.
Post a Comment