Nipo na Mama wa shoka huyu si mwingine ni; Mh.Anna Kilango Malecela, Mbunge wa Same Mashariki....huwa nampenda sana Mama huyu kwa kuchangamusha Bunge, analichangamsha sana tu! yupo mbele sana kwa kutetea wanyonge. Siku hii nilipohudhuria Bunge kwa kusikiliza Kikao na kutembelea Bunge, alinifurahisha sana maana alimtoa jasho sana Mh.Ngereja, Waziri wa Nishati na Madini...pale Mama huyu alipoikataa kabisa bajeti yake, na kuwa mkali sana tena sana....na kumwambia hata chai yako unayonipa ofa kila asubuhi siitaki kabisa, nitanunua mwenyewe chai hiyo, alichachamaa sana tena sana, Mh.Ngereja alinywea mwenyewe...na kweli bajeti ilikataliwa kupitishwa. Baada ya Kikao cha Bunge nilipata bahati ya kuonana naye Mama huyu Kilango na kumpa hongera zangu sana na kupiga naye picha.....na kutaniana maneno mawili matatu! Kwakweli Mama huyu wa Shoka sana, anastahili sana kuwa kiongozi hata wa ngazi za juu hana mchezo kabisa kutetea wanyonge.
No comments:
Post a Comment