Hapa tukiwa picha ya pamoja na Babu Marehemu Mzee Blezi....na watoto wake wawili wakiwemo kwenye picha hii ni; Andrea na Lucas...wengine wote ni wajukuu wa Babu, nikiwemo na mimi mwenyewe. Andrea ni wapili kushoto nyuma ya Babu, mwenye kofia. Lukas ni wa tatu kulia mwenye jaketi la bluu. Ukiacha Tall wa kwanza kulia...wote ni wajukuu kabisa wa Babu. Sikumbuki wajukuu tupo wangapi maana ni wengi sana...hapa ni wachache tu baadhi, Babu alikuwa na Watoto 8...na wote bado wazima, na wote wana watoto kibao....kasoro upande wangu mimi tupo wanne tu....wengine wote namba nyingi sana. Mjukuu Dino karibu na mimi mwenye shati ya milaba milaba...ana umri wa miaka 49, ana watoto 6...mtoto wake wa kwanza kwa jina Merania a.k.a Mere tayari ana mtoto wa miaka 2. Kwahiyo Babu ameona Kitukuu na kitukuu tayari kazaa, sijui wanamwitaje huyo...sijui Kilembe sina uhakika. Hivyo Babu kajaliwa kuishi miaka mingi na mwenye nguvu mpaka mwisho....ni jambo la kushukuru sana Mwenyezi Mungu.. kwa maisha yetu hasa ya vijijini sio rahisi sana kuishi hivi kwa muda mrefu. Kama hapa Kijijini kwa Babu...pagumu kweli, kwa kila kitu.
Babu ameacha watoto nane...wajukuu sijui wangapi, watoto hao ni;
1. Samweli
2. Jackson
3.Merania
4.Zita
5. Franco (Baba yangu)
6.Andrea
7.Lucas
8.Fabiani.
2 comments:
pole sana kaka kwa kufiwa na babu yako ni njia yetu sote hafadhali yeye hata ameona vitukuu na sisi wengine sijui itakuwaje hii ni njia yetu sote ni kumoombea tu MUNGU amlaze pema peponi nilikuwa nauliza hujaweza kujua hata babu amefikisha miaka mingapi?
Asante sana Mdau, kwa kunifariji kwako. Babu anahisiwa kuwa na kati ya 96 au zaidi ya hapo, si unajua tena zamani mambo yalivyokuwa kuhusu miaka, hasa vijijini hawakujua kabisa umri wao. Na Babu yangu alikuwa mmoja wa hawa ambao umri wao haukujulikana vizuri, kwa kukisiwa wanasema hivyo...mimi naamini hata 100 amefika.
Post a Comment