Gazeti la Mji wa hapa Cesena, almaarufu; IL RESTO DEL CARLINO CESENA.....na habari yetu ya Kontena la kwenda Tanzania. Habari ya mbele kabisa...basi leo simu yangu ilikuwa bize sana kila jamaa wa hapa Cesena wanaonifaamu; tumekuona kwenye Gazeti vipi eti sasa unarudi Tanzania kushika mambo haya? Ndo gazeti lilivyoandikwa, mara nikakimbia kununua Gazeti hili na kusoma habari yenyewe, nikakuta kweli wameandika maneno hayo, wakati mimi nilienda kusaidia tu, mimi nilikuwa hata sijui kama tutatoka kwenye gazeti....nilishituka sana baada ya kupokea simu ya kwanza na kuambiwa habari hii. Maana tulipiga picha za kawaida tu kama kumbukumbu...lakini nashangaa natokeza hapa, sikupenda sana lakiki basi, pia kutokana na habari ilivyoandikwa sio ya kweli sana kuwa mimi ndiye mtarajiwa wa Project hii Tanzania, na ninajiandaa kurudi hivi karibuni Tanzania.
No comments:
Post a Comment