Saturday, December 3, 2011

NITAMKUMBUKA MR.EBBO KWA KUJIVUNIA ASILI YAKE!


Huu wimbo huwa unanichekesha sana...oooh bado tunaunda kamati....oooh uchuguzi bado unaendelea!


Mbado hujaona Mzungu anaimba mipasho? (Taarabu)?......Mbado! na Samaki mkunje....kama waya!


Abel Loshilaa Motika a.k.a Mr.Ebbo, atakumbukwa sana kwa nyimbo zake alizoimba kwa maadhi ya matamshi ya Jamii ya Wafugaji kutoka Mkoani Arusha (Wamasai) ambako yeye mwenyewe ni asili yake. Miongoni mwa nyimbo hizo zilizo jizolea umaarufu miaka ya 2002 - 2004 ni pamoja na wimbo wa Mi Mmasai bwana, Kamongo, Unisamehe, Fahari yako, Njaa inauma, Bado kusungumsiwa.


Hakika kila aliyezisikiliza nyimbo hizi zikipigwa Redioni au zikichezwa katika Klabu na kumbi mbalimbali za starehe walivutiwa sana nazo na kiasi cha baadhi ya watu kutokana na upenzi wao katika nyimbo hizi walipewa majina ya utani kama lile la KAMONGO.

No comments:

WATEMBELEAJI