Sunday, December 4, 2011

MANENO MAZURI YA JUMAPILI YA 2 YA MAJILIO!

Enyi watu wa Sayuni, tazameni Bwana anakuja kuwaokoa Mataifa; naye Bwana atawasikizisha sauti yake ya utukufu katika furaha ya mioyo yenu.

Ee Mungu mwenyezi Rahimu, tunakuomba mambo ya dunia yasitupinge sisi tunaomkimbilia Mwanao tupate kumlaki, bali hekima yako itufanye tumshiriki yeye.

Ondoka...ee Yerusalemu...usimame juu; tazama uione furaha inayokuijia kutoka kwa Mungu wako.

No comments:

WATEMBELEAJI