Friday, December 2, 2011

TEDY..ALIYEKUWA BOSS WA WATER PROJECT - TANZANIA.



Hapa akiendeleza libeneke kama kawaida huko nchini Guatemala, Tedy alikuwa kioo kwetu vijana enzi hizo tukijifunza kazi, yeye alikuwa mkubwa wa Water Project...historia yake niliiandika hapa wiki iliyopita. Bado ni kakamavu wa kazi hizi za kusaka maji, baada ya kurudi kwao nchini Canada, nimepata taarifa zake bado anaendelea na kusaidia nchi zenye shida hasa kwa swala hili la Maji...mara nyingi huenda nchini Guatemala kwa kazi za visima na ujenzi wa matenki. Tedy ni kakamavu sana...anafanyakazi sana huyu jamaa.



Tedy ni nguvu kazi huyu Jamaa.






Tedy enzi zake akiwa Tanzania na uchimbaji wa visima na kazi mbalimbali za kijamii.






No comments:

WATEMBELEAJI