Friday, December 2, 2011

UKISEMA TUSILE UNGA....UGALI TUTASONGA NA NINI? MR.EBBO.



Nilikuwa nampenda sana huyu Jamaa Mr.Ebbo, nitaendelea kuwaleteeni nyimbo zake mbalimbali, ili tuendelee kumwenzi zaidi katika kifo chake hiki kilichotokea leo. Huu ni moja ya wimbo wake katika Albamu yake ya ALIBAMU, akisema; Ukisema tusile unga na ugali tutasonga na nini?


Miaka kama 4 iliyopita nilikuwa Mkoani Tanga....nilipanga kuonana na Mr.Ebbo kwa kusalimiana na kufahamiana tu, maana mimi ni moja ya mashabiki wake kwa muziki wake, niliweza kupata mawasiliano naye na tukapanga kuonana....lakini bahati mbaya mambo yaliingiliana na ikabidi nirudi Dar es salaam haraka, baadae nikarudi Italy, na ilikuwa kila niendapo likizo nashindwa kupata muda wa kwenda Tanga tena....nasikitika sana kwanini sikuweza kukutana nae....lakini basi ni mipango ya Mungu, nitazidi kumwombea ili aweze kupokelewa kwa Mwenyezi Mungu. Mungu amlaze mahali pema peponi Mr.Ebbo....amina!

No comments:

WATEMBELEAJI