Thursday, December 8, 2011
TUBURUDIKE NA NGOMA YA MGANDA - KUTOKA KWA WANGONI.
Tunapo jiandaa kusherekea miaka 50 ya Uhuru wetu hapo kesho....hebu tuburudike kidogo na ngoma hii ya mganda kutoka kwa Jamaa zangu Wangoni. Nilipokuwa Kijijini kwangu, hapo Parokiani tulikuwa na kikundi cha Ngoma....ambapo tulikuwa tunacheza ngoma mbalimbali, ikiwepo ngoma hii ya Mganda....tulifundishwa na Wangoni. Wangoni wengi sana wapo Kijijini kwetu, walikuja miaka ya zamani sana kwa kufuata uvuvi wa samaki, maana kuna Bwawa Kijijini hapo....walikuwa wakitufundisha kucheza, nami nilikuwa napenda sana ngoma hii mpaka hii leo hata kama sio mngoni wa kuzaliwa lakini hunishindi kwa kucheza mganda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
5 comments:
unasaema kweli siwezi kukushinda hata mimi mngoni kabisa kabisaaaa????
Wangoni Oyeeee!!!!!
OYEEEEEEEEEEEEE..MOJA, MBILI TATU..HAYA WUUUUU, WUUUUU, NA KUENDELEA halafu hapo unachukua stepu za maringo weeeweee
Hahhahahahha da'Yasintaaaaaaaaa!!!!
We Dada Yasinta...angalia vizuri eeh??? Unaweza usione ndani kabisa kwangu, Labda kwasababu sijacheza siku nyingi...kwasababu wewe ni ngoma yako ya asili huwezi kusahau tofauti na mimi niliyejifunza, lakini hata hivyo uwe mwangalifu sana kwangu naweza kukushinda mbali sana! au unabisha???
Post a Comment