Kamusi ya ''Oxford'' inatafsiri; kujiheshimu...kama mawazo mazuri kuhusu tabia ya mtu mwenyewe, iwapo anajiheshimu sana...maana yake ni kwamba; unajisikia vizuri. Unajua kwamba unayothamani - mtu unayestahili kupendwa...unajiheshimu mwenyewe.
Hisia za namna hii ni nzuri sana, unapojisikia kupendwa na kuheshimiwa unategemea hivyo hivyo kutoka kwa mtu mwingine vile vile. unajiheshimu sana haina maana ya kwamba; wewe huwezi kujichukia au kujikasirikia mwenyewe. Kuna wakati kila mtu hukata tamaa, lakini yule mwenye kujiheshimu anakubali makosa na kusonga mbele. Kujiheshimu ni tofauti kabisa na kujidai au kuwa na majivuno mengi. Watu wanaojienzi - wanajipenda, lakini haina maana ya kwamba wanajifikiria wao hawana dosari yoyote, au wao ni bora kuliko wengine. Fikiria wewe ni mtu wa aina gani na kutengeneza orodha ya sifa ulizonazo. Unapenda nini kuhusu wewe mwenyewe? Wema wako? Ucheshi? Ubunifu? Umakini?.....Halafu mambo yanayokuhusu ambayo ungependa kuyaboresha, lakini usijikosoe sana....kuwa mhalisi na weka malengo ambayo yanatekelezeka na yatakayo onyesha mafanikio ili uridhike unapoyakamilisha....jiamini na jiambie; ''Nimeweza''.
Tumia muda wako na watu wanaokujali, wanaokufanya ujisikie vizuri na kuongeza hadhi ya kujiheshimu. Kaa mbali kabisa na watu wanaojaribu kuharibu heshima yako, hasa kama wanafanya hivyo kwa sababu fulani. Kwa vyovyote vile kuifanyia kazi heshima yako haina maana kuwa hutaweza kupata matatizo....kuifanyia kazi heshima yako itakusaidia matatizo kuwa mepesi. Kujiheshimu kunakulinda wewe mwenyewe binafsi.
- Ukijiheshimu unajua jinsi ya kugombana na kusimamia unachokiamini kwa heshima!
No comments:
Post a Comment