Monday, January 16, 2012

IBADA YA KUMWOMBEA MH.MBUGE REGIA MTEMA...HII LEO!

Mhashamu Askofu Salitarus Libena, ambaye ameteuliwa hivi karibuni kuwa Askofu wa Jimbo jipya la Ifakara, ambaye mpaka sasa ni Askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam...leo hii aliongoza Ibada ya Misa Takatifu ya Wafu ya Mh.Regia Mtema, Mbunge wa Viti Maalumu Chadema, aliyefariki kwa ajali ya Gari katika eneo la Ruvu - Pwani.
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Anne Makinda, akitoa salamu zake za mwisho mbele ya Jeneza la Mh.Mbunge Regia.
Mwenyekiti wa Kambi ya Upinzani Bungeni, pia Mbunge wa Hai kupitia Chadema, Mh.Freeman Mbowe, akitoa salamu zake za mwisho mbele ya Jeneza la Marehemu Mbunge Regia.
Waumini wakipita mbele ya Jeneza la Marehemu Regia, kutoa salamu zao za mwisho.

No comments:

WATEMBELEAJI