Leo nikiwa katika mkutano hapa kazini kwangu, mkutano huo kati ya Boss wetu na sisi Wafanyakazi....wafanyakazi walichachamaa kuhusu swala fulani la haki zao mpaka nikaogopa, Boss mwenyewe alijieleza na kuwa mkali....lakini alishindwa akalegea mwenyewe mpaka unamwonea huruma. Wafanyakazi wa huku Ugaibuni sio mchezo, katika haki zao hawana utani kabisa.
Wakati mkutano huo wa mabishano hayo unaendelea, nikawa nawaza sana....jambo kama hili lingekuwa Tanzania je ingekuwaje? Sio wote tungefukuzwa kazi kabisa, maana huko kwetu haki hamna kabisa kuhusu wafanyakazi....tena ukileta mchezo siku hiyo hiyo unafukuzwa na unaona mtu mwingine anashika kazi yako hivi hivi ukiona.
Mimi siku moja nikiwa Tz, kwenye mkutano kama huu wa Wafanyakazi nilijaribu kutetea kitu fulani cha haki kabisa kwa kuuliza swali tu, nikajibiwa kama hupendi kazi endelea na maswali yako hayo utaona mwenyewe. Hivi kwanini huko kwetu tunakuwa hatuna haki kabisa makazini kwetu? Sheria za kazi zipo kabisa, lakini hazizingatiwi kabisa......na waajili wengi wakiona unafuatilia sana sheria hawakosi kukutimua.
- Kweli kabisa msemo huu usemao; SHERIA DUNIANI HAKI MBINGUNI.
No comments:
Post a Comment