Thursday, January 12, 2012

KUTOKA KAMBI MPYA ZA WAATHIRIKA WA MAFURIKO YA DAR.

Wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania, wanaotoa huduma mbalimbali katika kambi za Waathirika wa Mafuriko ya Jijini Dar es salaam...wakiandaa ugali wa mchana katika eneo la Mabwe Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam...ambako baadhi ya Waathirika hao wanaandaliwa viwanja na makazi yao ya muda.
Hapa ugali unaonjwa kama upo tayari (umeiva) kwa kuliwa.
Mahema yaliyo kamilika yaliwekwa Nembo maalum za Shirika hilo la Msalaba Mwekundu.
Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania, limetoa Mahema zaidi ya 200 katika eneo hilo la Mabwe Pande, ambayo tayari yamefungwa eneo hilo husika kusaidia wahusika hao wa Mafuriko.

No comments:

WATEMBELEAJI