Mabibo ya korosho yanaachwa yakioza, wakati yakikamuliwa yanatoa juisi bora na nzuri tu!Ziara ya Wataalamu wa Pembejeo kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, iliyofanya hivi karibuni ziara hiyo katika Mikoa inayozalisha Korosho nchini, imebaini kuwa matunda ya korosho (Mabibo) bado yanaachwa yakioza mashambani.
Kwanini yanaachwa....ni kutokana na desturi ya tangu zamani ya Wakulima wa Korosho kutothamini Mabibo na hivyo kuyaacha yakioza ardhini bila ya kuyakamua kienyeji na kutengeneza Juisi. Katika ziara hiyo, Wataalamu hao...Rose Kitambi na Anderson Tweve, walisema; Wananchi wanatakiwa kubadilika na kuacha utamaduni wa kuyatelekeza mabibo shambani badala yake wasafirishe na kupeleka viwandani kukamuliwa Juisi na Mvinyo.
- Habari na Magnus Mahenge.
No comments:
Post a Comment