Sunday, January 8, 2012

MANENO MAZURI YA JUMAPILI HII YA EPIFANIA.

Tazama anakuja Mtawala Bwana, mwenye ufalme mkononi mwake na uweza na enzi.

Tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja na zawadi kumsujudia Bwana.

Niliona mtu ameketi katika kiti cha enzi cha mbinguni. Malaika wengi walimwabudu mtu huyu, wakiimba pamoja; Tazama, jina la ufalme wake ni la milele.

Ee Bwana tunakuomba uzikubali kwa neema sala za taifa lako, tupate kutambua yatupasayo kutenda, tuweze kuyatimiza hayo tuliyoyatambua.

No comments:

WATEMBELEAJI