Tuesday, January 17, 2012

MH.MBUNGE MAREHEMU REGIA MTEMA ENZI ZA UHAI WAKE!

Mh.Regia Mtema, ambaye enzi ya uhai wake alisifiwa kwa ujasiri, upole na uwezo mkubwa wa kujenga hoja kwa sauti nyororo isiyo na jazba. alifikwa na mauti baada ya gari lake aina ya Toyota Land Cruiser VX, kupinduka mara saba.
Rogers Abdallah, ambaye ni majeruhi wa ajali hiyo...alisema; Mh.Regia ndiye aliyekuwa akiendesha gari hilo, tulikuwa tukienda shambani Ruvu....tulipofika Ruvu darajani, alitaka kulipita lori lakini alipoanza tu kulipita tukakutana na lori jingine uso kwa uso, ili kulikwepa lori hilo ikabidi apandishe kulia kwa kulitoa gari nje ya barabara, bahati mbaya tairi la mbele la kushoto likapasuka hivyo gari likapinduka mara saba, ''alisema hivi Rogers''

Marehemu Mbunge Regia, alikuwa mlemavu wa mguu wa kulia, ilikuwaje akaendesha gari? aliulizwa hivi Rogers. Alijibu hivi; Mara kwa mara mimi ndiye huwa namwendesha, lakini leo alisema; anaendesha mwenyewe na akichoka ndipo nitamwendesha....basi ikawa bahati mbaya, alisema haya Rogers.

- Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi.....amina!

No comments:

WATEMBELEAJI