Mwanafunzi wa Kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Edmubdrise, inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Arusha.....John Justine (17) amejiua kwa kujipiga risasi kifuani. John amejiua kwa kutumia bunduki aina ya Shotgun ya Baba yake mzazi Justine Kaiza, baada ya kutuhumiwa na Baba yake huyo kuwa amemwibia fedha taslimu dola za Kimarekani 1,500.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye....amethibitisha kutokea habari za kujiua kwa John, na kusema alifanya hivyo juzi usiku majira ya saa 1:30 katika eneo la Makao Makuu mapya Kata ya Levolosi Jijini Arusha.
Polisi wanamshikiria Baba wa Marehemu kwa mahojiano kuhusu kifo hicho na umiliki wa bunduki hiyo kwa kuwa inadaiwa na ndugu wa Familia kuwa John aliuawa na Baba yake huyo kutokana na upotevu wa pesa hizo pamoja na madai kuwa bunduki hiyo haimilikiwi kihalali.
- Habari na Mdau John Mhala - Arusha.
No comments:
Post a Comment