BAADHI YA VIJANA WALIOPO KITUO CHA ALLIANCE SPORTS ACADEMY.Mkoa na Jiji la Mwanza ni miongoni mwa Majiji yenye utajiri wa vipaji vilivyojificha vya kusakata soka. Ukweli huu unathibitishwa kutokana na kuwepo kwa baadhi ya Wachezaji waliowahi kuvuma na wanaendelea kuvuma hadi sasa katika medani ya soka wakitokea Jijini Mwanza. Lakini wakati Jiji hili likiwa na utajiri huu mkubwa, bado medani ya soka ingali bado ikisuasua tu!
Hii ni kutokana na kutokuwepo kwa juhudi mathubuti miongoni mwa Klabu na Wadau wa soka kwa ujumla katika kuendeleza vipaji vilivyopo. Nakumbuka katika miaka ya 1980 Mkoa wa Mwanza ulikuwa katika ramani ya soka Kitaifa ilipokuwa Timu na Wachezaji mahiri waliotamba enzi hizo. Baadhi ya Timu zilizovuma Mkoani Mwanza ni; Toto African, Co-op United, Mzalendo United, Maji Mwanza, Polisi Mwanza na Lumumba Rovers.
Wachezaji waliovuma enzi hizo ni; Athuman Juma Chama (Jogoo) aliyetokea Bugarika Shule ya Msingi, alichezea Yanga na Taifa Stars, na wengine akina Mrisho Ngasa, ambaye kwasasa anaichezea Timu ya Azam FC na Jerryson Tegete, ambaye yupo Yanga. Hao niliowataja kimsingi wanatokea Mkoani Mwanza.
- Habari na Nashon Kennedy.
No comments:
Post a Comment