Mazoezi ya Timu ya AC.Milan ya Italia, katika ufukwe wa bahari ya; AL-MAMZAR BEACH IN THE GULF EMIRATE OF DUBAI. Wachezaji hawa wa Ac.Milan wakiwa likizo ya Krismas na Mwaka Mpya huko nchini Dubai. Baharini kulikuwa na watu wengine pia, kama akina dada ambao waliwaacha wachezaji hawa; wakishangaa na kutamani akina dada hao baharini hapo, macho yote ya wachezaji hawa kwa akina dada.
Katika tizi la kukimbia, katika ufukwe wa Bahari huko Dubai.
Wakishangaa akina dada wazuri, Baharini hapo.
Huyu Dada ndio chanzo hasa, cha wachezaji wa Ac.Milan, kushangaa na kujisahau na mazoezi yao; Dada mzuri huyu duuuhh...!!! ngoja tushangae kidogo jamani.
Kazi kweli kweli....mpaka mazoezi yanasimama, Ac.Milan mtakuja kufungwa na wenzenu wanaojifua kisawasawa bila kushangaa akina dada....haya shauri yenu. Mimi ni shabiki mkubwa wa Ac.Milan, msiniangushe vijana!
Mchezaji Robihno....taratibu jamaa yangu! Mwishowe utasahau hata mazoezi.
Robihno, akipumzika kidogo baada ya mazoezi na kushangaa vimwana.
Kipa mashuhuri sana wa Ac.Milan, Cristian Abbiati..kushoto na beki Mexes, wakipumzika kidogo baada ya mazoezi, baharini Dubai.
No comments:
Post a Comment