WANANCHI WAKABIDHIWA DARAJA LA MABANZI - MBEYA!
Wananchi wa Kitongoji cha Kinyasuguni, Wilayani Mbarali, Mkoani Mbeya....majuzi wamekabidhiwa rasmi daraja lenye urefu wa zaidi ya Mita 500. Daraja hilo limejengwa kwa magogo na mabanzi, lipo katika Bonde la Usangu...likiunganisha Kitongoji hicho na kile cha Mahango, vinavyotenganishwa na Mto Lyandembera, katika eneo maarufu la kilimo cha Mpunga - Madibira.- Picha na Habari na Frank Leonard.
No comments:
Post a Comment