Mwenyekiti wa Kijiji cha Kapunga, Bwana Ramadhani Nyoni....akionyesha turubai ambalo lilitumika kufunika mbegu na kisha kunyunyiziwa.
Mtoto huyu alikuwepo shambani wakati Mwekezaji alipomwaga sumu mashambani.
Miguu ya Bwana Benjamini Hebel (44) mmoja wa Wakazi wa Kijiji cha Kapunga, Wilayani Mbrani, Mkoani Mbeya.....ilivyoharibika baada ya Mwekezaji wa Kapunga Rice Project, Bwana Wally Vermaak.....kumwaga sumu kwa kutumia Ndege katika mashamba ya Wananchi kufuatia mgogoro wa kugombania ardhi baina ya Wananchi na Mwekezaji huyo.
Sehemu ya mimea ya Mahindi na Mpunga iliyonyauka katika Mashamba ya Wananchi wa Kijiji cha Kapunga, baada ya kumwagiwa sumu na Mwekezaji wa Kapunga Rice Project Bwana Wally Vermaak.
Kibanda kinasadikiwa kilimwagiwa sumu na Mwekezaji huyo, licha ya Wananchi kujihifadhi ndani ya Kibanda hicho.
Baadhi ya Wananchi walioathirika na sumu iliyomwagwa na Mwekezaji, katika mashamba yao na kisha kula mboga iliyomwagiwa....hali iliyopelekea kuhara.
No comments:
Post a Comment