Friday, April 6, 2012

LEO NI SIKU YA IJUMAA KUU......TUKUMBUKE KWA KUSALI.

Ijumaa kuu, tukumbuke kwa kusali na kufunga!

Tutazame kwa makini maana ya kilio cha Yasu msalabani; ''Mungu wangu.....Mungu wangu'' mbona umeniacha? Sala aliyoitoa baada ya kupita saa tatu ya kipindi cha giza kilichoikumba dunia nzima.
Mara nyingi giza hutumika kama ishara ya uweza wa mwovu, na pia inaweza kutumika kuonyesha fumbo la uwepo wa Mungu. Mfano; Musa....alifunikwa na wingu la giza, hivyo hivyo Yesu akiwa Karvario alifunikwa na wingu la giza. Ingawa Yesu akiwa msalabani alionekana kama vile ameachwa na Baba, bado upendo wa Baba......ulikuwa pamoja naye, akimtazama Mwanae kwa makini, katika mateso na mahangaiko ya kumkomboa binadamu.

No comments:

WATEMBELEAJI