Thursday, April 5, 2012

SWALI LA MJENGWA; KUNA WALIO PITIA HAPA?


Mkuu Mjengwa, na mimi nakujibu swali lako;
Ndio kuna waliopitia hapa, nikiwemo mimi mwenyewe......nimepitia hapa! Tena umenikumbusha mbali sana, nilikuwa na rafiki yangu mpendwa sana tukiwa pamoja hapo Kigurunyembe, tumepotezana kabisa......sijui yupo wapi, jina lake; Clarence Mkwavi......nimefanya kila binu ili nimpate lakini wapi.
Kigurunyembe napakumbuka sana na kasheshe zake, baadae nilihama.....nikahamia Dar, pale Tegeta Sec......walimu na wanafunzi wenzangu, wakaanza kuniita jina hili la Kigurunyembe, ilikuwa kila wanionapo utasikia; we Kigurunyembe! Kwasababu nilitokea Kigurunyembe...........pia kwasababu nilibaki na nembo ya Kigurunyembe katika shati langu la shule......mwanzo nilikuwa nikikasirika sana, baadae nilizoea!

No comments:

WATEMBELEAJI