Sunday, April 1, 2012

WANAFUNZI WA UDOM WATOA ZAWADI YA PASAKA KWA WATOTO YATIMA WA MIYUJI - DODOMA!

Wanafunzi wa Chuo cha UDOM....watoa zawadi ya Pasaka kwa Kituo cha kulelea Watoto yatima cha Miyuji - Dodoma.
Hii ni moja ya picha kubwa iliyochorwa katika ukuta wa bweni ambalo wanalala watoto yatima hao.
Mbuzi akiwa amepakiwa kwenye daladala, mbuzi huyo alikua ni moja ya zawadi ya Pasaka kutoka kwa Wanafunzi wa UDOM.
Wanafunzi wa Chuo cha UDOM wakiwasili katika Kituo cha Watoto yatima cha Miyuji, na kiroba cha unga kama moja ya zawadi walizowapelekea watoto hao.
Watoto waishio katika Kituo cha kulelea Watoto yatima, wakiwa wamekusanyika kwa furaha kupokea zawadi kutoka kwa Wanafunzi wa UDOM....baada ya Wanafunzi hao wa UDOM kuwasili Kituoni hapo.

Wakicheza pamoja kwa furaha.....

Picha ya pamoja; baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha UDOM wakiwa pamoja na Watoto yatima wa Miyuji - Dodoma.

- Picha na Lukaza.

No comments:

WATEMBELEAJI