Friday, February 1, 2013

HIVI MTU ANAYEFANYA HIVI NI MZIMA WA AKILI KWELI?

Nimekutana na hii picha Facebook, na nimebaki na mshangao kuona mtu amemweka huyo mtoto kwenye Photocopy Mashine ambayo inawaka. Sijui ni mzazi ama mlezi, nahisi ni mpumbavu sana na akili zake hazimtoshi hata kidogo. Huwezi mfanyia mdhaha mtoto katika mashine ya umeme tena ukizingatia mionzi yake ni mikali sana. Inasikitisha sana, mtoto wala hajui lolote.....lakini hao wakubwa wanamfanyia ushenzi tu! 
- Jamani tusichezee watoto kwa masihara masihara tu! kuna watu wanawatafuta usiku na mchana hawawapati hawa watoto, kama hutaki watoto basi acha kuzaa.

No comments:

WATEMBELEAJI