Tuesday, October 21, 2014
FR.MAKWANDA - C.PP.S. MPENDWA WETU UMETUACHA.
Rafiki yangu mpendwa sana Fr.Makwanda, wa Shirika la damu azizi ya Yesu (C.PP.S)......hata bado siamini kabisa kama haupo nasi tena hapa duniani, lakini inabidi tu niamini...ajali yako mbaya ya gari imetuumiza sana hata hatujui tufanye nini, umetuacha bado kijana kabisa...tulikuwa tunategemea sana, huduma yako sana katika Kanisa na jamii kwa ujumla. Kwakweli katika hali ya kibinadamu inauma sana, maana kifo cha ajali kinauma sana. Mimi pia inaniuma zaidi maana siwezi hata kuhudhuria mazishi yako hapo Manyoni Ijumaa asubuhi, maana Jumamosi mchana nitakuwa safarini kwenda Italy.....hivyo naumia sana, lakini basi sina budi kukubali tu. Ninakuombea sana kwa Mwenyezi Mungu mpendwa sana rafiki yangu Makwanda. Mwenyezi Mungu akupumzishe kwa amani Fr.mpendwa wetu Makwanda.
- Roho ya milele umpe ee Bwana.......na mwanga wa milele umwangazie.......apumzike kwa amani Padri wetu mpendwa Makwanda......Amina!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Ni masikitiko kumpoteza Jirani yangu Biri malinyi ukanga Poleni wakina Judy
Post a Comment