Mtangazaji mahiri sana wa Radio ya Ebony Fm ya Iringa.....ni mtangazaji anayevutia sana na kuchekesha sana anapokuwa kwenye vipindi vyake, nimemsikiliza mara nyingi nikiwa pale Mafinga ki kazi, kwakweli lazima ucheke na kufurahi sana hasa pale anapoongea na kuchanganya maneno na kilugha chake (Kihehe) inaleta raha sana kuona jinsi anavyo jali na kudumisha mila na tamaduni za kabira lake la Kihehe.....na kujali sana lugha yake ya Kihehe ambapo sisi wengine tunazikana mila na tamaduni zetu na kuogopa kuongea kilugha machoni pa watu (Hadharani).
Kwakweli hongera sana Dj....kamanda Eddo.
No comments:
Post a Comment