Saturday, October 15, 2016

HII KWA WADAU WOTE WAPENDA SOKA WA WILAYA YETU YA MANYONI.




Wadau wenzangu wapenda soka kama mimi wa Wilaya yetu ya Manyoni....tuna timu yetu nzuri ya Wilaya, lakini tunaisapoti vipi hii timu yetu? Au tunabaki kushangilia timu nyingine tu? Kwanini tusiipenguvu zaidi timu yetu kwa kuchangia walau ulichonacho kwa kila mwezi, tukomaee mpaka ifike ligi kuu, kwani nyingine ziliwezaje?....ni mawazo tu, mpo wana Manyoni wenzangu wapenda soka?

Kesho Jumapili ya tarehe 16/10/2016....timu yetu itacheza  mechi ya kirafiki na timu ya Itigi, ijulikanayo kama Small Boys....hata hii ni timu mojawapo ya Wilaya yetu...zitacheza katika Uwanja wa Jumbe hapo Manyoni mjini, wote tunakaribishwa kushuhudia mpambano huo, pia ukichangia hata maji wakanywa wachezaji wetu itakuwa ni nzuri zaidi. Mimi binafsi nategemea kwenda kesho Manyoni nikitokea hapa Dodoma.

- KARIBUNI SANA WADAU WA MPIRA MANYONI.

No comments:

WATEMBELEAJI