Sunday, October 16, 2016
MWEZI WA ROZARI TAKATIFU....TUWE DAIMA NA MAMA YETU MARIA. JUMAPILI NJEMA KWENU NYOTE!
Ungekuwa bendera Mama Maria, ningekuweka kwenye mlingoti.....ili watu wote wauone uzuri wako na upendo wako Mama.
Ungekua kengere Mama Maria, ningekugonga kila asubuhi......ili watu wote duniani waweze kukuheshimu Mama.
Ungekuwa kinanda Mama Maria, ningalikucheza kila siku.....ili watu wote wasikie uzuri wa sauti yako Mama.
Ungelikuwa ni nguo Mama Maria, ningali kuvaa kila siku......ili watu wote waone uzuri wa maua yako Mama.
Ungalikuwa mafuta Mama Maria, ningalijipaka kila siku......ili watu wote wasikie marashi yako Mama.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment