Friday, October 14, 2016

MTUMISHI WA MUNGU MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE!


Mtumishi wa Mungu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, sasa ni miaka 17 tangu ututoke duniani, twakukumbuka sanaa Baba yetu, twakumbuka utumishi wako ndani ya Kanisa na katika Serikali yetu.

Hekima zako Baba hatutazisahau kamwe, tutakukumbuka milele yote na hata vizazi vyote daima!

Imani yako Baba na unyenyekevu wako ndio siraha yetu tuliyonayo Tanzania ndiyo tunajivunia daima hata sasa.

Amani uliyopanda miyoyoni mwa waTanzania ni kitu kikubwa sana cha kujivunia katika Taifa letu na hata duniani kote!

Urithi wa imani na umoja wa dini zetu, hii ni hekima yako Baba, na leo hii tunafaidi matunda haya mazuri sisi wanao waTanzania.

Baba uliahidi kutuombea daima kwa Mungu, endelea kutuombea...ili tuendelee kupambana vilivyo, ili tuyafikie malengo kama ulivyokuwa ukitamani wewe siku moja iwe hivyo kadiri ya matamanio yako Baba.
Mtumishi wa Mungu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere utuombee......amina!

Endelea kupumzika kwa amani Baba yetu mpendwa wetu.

HESHIMA YA MTU NI UTU WAKE...SI MALI WALA CHEO!
''AMANI HULINDWA KWA KUTENDA HAKI''

MUNGU MBARIKI BABA YETU MPENDWA SANA MWALIMU NYERERE....MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE WOTE!

No comments:

WATEMBELEAJI