
Waziri Mkuu Mh.Mizengo Pinda, majuzi alitaja mali anazomiliki ambazo miongoni mwake ni nyumba mbili pamoja na akaunti katika benki zenye fedha zisizozidi milioni 25. ''Kama shilingi milioni 25 ni utajiri basi nami nimo'' alisema hivyo Waziri Mkuu ofisini kwake, Magogoni - Dar wakati akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari vya ndani ya nchi.Pinda amesema anamiliki nyumba moja mjini Dodoma na nyingine kwao Mpanda mkoani Rukwa eneo la Makanyagio, na ana kibanda shambani kwake Pungu nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
''Mimi kila mwaka nataja mali zangu kwa Tume, sijaulizwa, sijagombana na Tume.'' Ukiniuliza ni masikini kiasi gani, nitakwambia nina property (nyumba) Dodoma nimejenga kwa utaratibu wa serikali wa kuomba mkopo, ninayo nyingine kwetu Mpanda pale Makanyagio, ''alisema Pinda''.
Dar es salaam sina nyumba, pale Pugu nina nyumba kidogo inahitaji kazi ya ziada, kijijini nilikuwa nafikia kwa Babu, Babu ana kanyumba kake ka ovyo ovyo kile ambacho mlikiona, ana vyumba viwili nilikuwa nalala pale, lakini baada ya uwaziri mkuu, jamaa wakaniambia aah...haiwezekani pale, nilijua nitaweza kulala pale na hawa jamaa (wasaidizi wake) watalala mjini Hotelini, nikaambiwa hapafai.
Pinda ambaye pia ni mbunge wa Mpanda mashariki alisema hana gari lolote zaidi ya gari alilopewa kwa kuwa mbuge, na kwamba katika akaunti zake zote ana fedha kiasi cha sh. milioni 25. Lakini mkubwa Pinda alisema kwamba kwa jinsi serikali inavyowajali watu wanaoshika wadhifa kama wake, haoni ni kwanini awe na tamaa ya fedha na mali, kwasababu serikali inamjali kwa kumtunza kwa kila kitu. Kwa utaratibu wa serikali unapewa nyumba, magari, unalishwa na serikali... kwa mshahara wake unaweka akiba ya kutosha, unataka utajiri wa nini? Maisha yako ni mazuri, unataka nini zaidi ya hapo? Ukitoka nje ya utumishi wa serikali akiba yako inakusaidia kusomesha watoto wako, ''alifafanua Waziri Mkuu'' alisema hana sababu ya kuwa na tamaa, jukumu lake kubwa aliloomba kwa Mwenyezi Mungu ni kumpa uwezo wa kuwatumikia watanzania vizuri zaidi. Sina hisa popote, labda huko mbele ya safari nitafikiria. Yaani ukiwa Waziri Mkuu ndio mwanya wa kujinufaisha, kwanini? Labda mimi watu wanaweza kusema Waziri Mkuu wa sasa ni mjinga,''aliongeza Pinda. Nipo kwaajili ya watu, kuwatumikia si kujinufaisha mwenyewe.
-HONGERA SANA KWA WAZIRI WETU MKUU, NASI TUNAKUOMBEA ZAIDI NA ZAIDI UDUMISHE UAMINIFU WAKO HUO SIKU ZOTE. NA TUNAKUOMBEA HAPO BAADAE UWEZE KUWA RAIS WETU.
No comments:
Post a Comment