Monday, April 12, 2010

KWELI KABISA BONGO NI TAMBARARE HAWAKOSEI.

Mara nyingi vitokeapo vifo vya ghafla, huwa mawazo yetu yanakimbia amerogwa huyo,...amerogwa wapi?? hatukumbuki hata mzingira tunayoishi kuwa yanatutatiza afya zetu na kutukatisha maisha mapema. Vyanzo vyake pia ni kama hapa tuonavyo..mazingira magumu, hapa magonjwa yanalipuka kama utani vile. Mbona kwa wenzetu hayatokei kama haya? pia ukiangalia wana maisha marefu...unafikiri maisha marefu yanatokana na nini? Ee Mwenyezi Mungu endelea kutulinda na kutuepusha na magonjwa, maana ndio wewe pekee unayeweza kutuepusha na haya majanga. Hii barabara inaelekea machinjio ya Ukonga.
Hapa maswali ni mengi sana...na majibu ni machache sana.
Acha tuone.

Hapa si utani wakati huu wa masika uongozi wa Kata ya Ukonga uliopo jirani kabisa na eneo hili, ujipanga vema kwa ajili ya huduma za Jiji na Manispaa ili madhara katika eneo hili yasiongezeke.
Hapa ni sokoni na madukani kwa ajili ya mahitaji muhimu, je afya zetu zinakuwaje hapa?
Wadau wa Mombasa na Mazizini mnasemaje?

-Ray Njau.

No comments:

WATEMBELEAJI