Sunday, April 11, 2010

LIGI ZENYE UWEZO WA KUHIMILI MIKIMIKI YA AGA LA KIMATAIFA.

UBUNIFU WA MFUMO WA LIGI ZENYE UWEZO WA KUHIMILI MIKIMIKI YA ANGA LA KIMATAIFA.

Hapa hakuna haja ya kutafuna maneno kuhusu mfumo wa ligi nchini Tanzania kuwa hauzisadii kabisa timu za ligi kuu kuingia kwenye mikimiki ya ushindani barani Afrika. Kwa ujumla naona ligi zetu hapa mashariki mwa Afrika zimepooza sana na hata wale wadhamini wa ligi hizi hawapo kwa ajili ya manufaa ya ligi husika bali kwa promosheni zao za kibiashara tu. Kufikia wakati huu hakuna sababu ya msingi sana inayoweza kuelezea kwa nini michezo ya ligi kuu nchini Tanzania haionyeshwi moja kwa moja kwenye vituo vya televisheni.

Mshangao mkubwa ni vile vikao na mikutano ya siku wadau wa soka ambayo inaendelea kila siku. Mikutano hiyo imeshindwa kabisa kutoa dira na mwelekeo mpya wa kuifanya Tanzania kuingia kwenye ramani ya soka barani Afrika.

Tafadhali sana wadau wa soka tujadili kwa mapana umuhimu wa kuwa na ligi zenye ushindani wa kweli unaoweza kuhimili mikimiki ya kimataifa na siyo kuishia kwenye lizombe na mdumange kila mwisho wa msimu wa ligi.

Mdau wa Michezo
Dar es salaam.

1 comment:

ray njau said...

Wadau wa soka tumechoshwa na kuendelea kuwapigia wenzetu makofi kila siku na sasa tunataka ligi kuu yenye ushindani wa kweli na siyo ushabiki na utani wa jadi.

Kwa sasa naamini tuweza kupata changamoto mpya iwapo tutaamua kuwa na ligi ya timu za majeshi ya ulizi na usalama.

Kupitia ligi hii tutaweza kuibua vipaji vipya vyenye nidhamu na ukakamavu wa kutosha.

WATEMBELEAJI