Monday, May 24, 2010

KULEA WATOTO SI KAZI NDOGO: SI MCHEZO KABISA!

Jamaa yangu Reggi hapo pembeni, alikuwa akinicheka sana maana nilikuwa nikimshika tu mototo analia kweli kweli...!!! lakini yeye akimchukua ananyamaza. Kulea si mchezo! lakini nilivyokuwa mdogo nilimlea mdogo wangu Josephina vizuri bila shida yoyote. Ila sasa sikumbuki tena, maana mama yangu alikuwa akienda shuleni kufundisha ananiachia mtoto nyumbani, ambaye ni mdogo wangu Josephina, na alikuwa na fujo za kila aina Josephina lakini niliweza kukabiliana nae vizuri bila shida yoyote na nilikuwa mlezi mzuri tu! Kwasasa nimepoteza uzoefu huo wa kulea watoto, itabidi nianze tena kufanya zoezi hilo.
Hapa tulikuwa Arusha kwa rafiki yetu mmoja, mwaka jana tulipoenda kumtembelea na kumpa hongera ya kupata mtoto.

-Hongereni sana akina Mama na Walezi wote kwa kazi nzuri ya malezi ya watoto.

No comments:

WATEMBELEAJI