Wednesday, May 12, 2010

WATU NA TABIA ZAO KAMA ZA UMBU!

...nilihudhuria maziko ya mama mkwe wa mdogo wangu alifariki kwa tatizo la INI akiwa na miaka 84 huko kijijini kwetu. Ni maziko ambayo hayakuwa na vikorombwezo kibao kama mapicha ya video n.k. Mashada nayo yalikuwa ya kawaida ambayo yalitokana na miti na nyasi zilizokatwa na kukunjwa kiaina.

Maziko yaliendeshwa na Padre ambaye ni Paroko wa Kanisa - mahali, na nimevutiwa sana na sehemu ya mahubiri yake kwa jamii ya kileo.

MBU: Paroko alisema; sasahivi watu tunaishi kama MBU katika jamii. Mbu tabia yake ni kueneza ugonjwa wa malaria. Kwa usiku mmoja anaweza kueneza kwa watu lukuki, watoto, wamama, wababa, wazee n.k.

Jamii yetu nayo imekuwa hivo hivo, maisha tunayoishi yamekuwa kama ya mbu ya kueneza magonjwa. Mahusiano kati ya mtu na mtu yako hovyo, mtu anaweza kugobanisha mtaa ama ofisi nzima kwa fitna na majungu. Na inakwenda mbali na hapo: mtu sasa anajifitinisha yeye mwenyewe katika nafsi yake!

Je, katika mazingira yako, wewe ni mbu?

1. Mtu mmoja mmoja: je unatimiza wajibu wako katika familia, pahala pa kazi, jamii n.k?

2. Chama cha siasa, wewe ni mbu? Unaeneza siasa za chuki na mafarakano katika jamii badala ya upendo, amani na mapatano?

Je unahubiri uwazi, uwajibikaji, n.k, wakati wewe unafanya tofauti kwa kukumbatia ufisadi?

-Chacha Wambura
Kwa hisani ya WAVUTI.

No comments:

WATEMBELEAJI