Saturday, May 22, 2010

WEEKEND NJEMA NA JUMAPILI NJEMA SANA KWENU NYOTE!

BURUDIKA NA WIMBO MZURI WA; MWOKOZI WETU YESU. KUTOKA KWA; MED MEDRICK SANGA.

UJUMBE WA LEO:

SIFA KWAKO BWANA;

Nitatumia midomo yangu kukusifu Ee Bwana, nitatumia ulimi wangu kukuimbia sifa nyingi sana, nitaimba nyimbo nzuri kwa kinanda na ngoma, nitatumia vipaji vyangu kukusifu Ee Bwana Mungu wangu.

Nitatumia miguu yangu kukutafuta Ee Bwana, nitatumia magoti yangu kukuabudu Ee Bwana, nitakwenda pande zote kati ya Mataifa, nitatumia uhai wangu kukutafuta Ee Bwana Mungu wangu.

Nitatumia Imani yangu kumshinda shetani, nitatumia sauti yangu kukemea maovu na nitatumia hekima yangu kuwakusanya wote. Mungu Baba, Mwana na Roho mtakatifu mnilinde na kuniongoza vema, na watu wote Duniani.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nawe pia kakangui na wengine wote!!

Anonymous said...

Asante Chibiriti,
mimi nasubiri jambo moja muhimu sana toka kwako. Naomba tuwekee tena wale watangazaji mashabiki wa Inter Milan wakitangaza "goal goal goal goal! Militooooooooooooooooooooooooo. Mimi ni shabiki mkubwa wa Mourinho na najua sasa akitoka hapo atakuja kwa timu yangu niipendayo kabisa "RM"

WATEMBELEAJI