Wednesday, June 2, 2010

HAPA NILIPO NAKUNA KICHWA MPAKA KICHWA KINANIUMA.

Nakuna kichwa mpaka kichwa kinaniuma, sipati jibu!

Rafiki yangu sana, (wakaribu sana) Isabella wa huko mji wa Imola, km 50 toka hapa Cesena. Ameniomba sana niwafundishe wimbo wa Kiswahili watoto wa shule ya msingi afundishayo, maana yeye ni mwalimu wa shule ya msingi, na anasema siwezi kukwepa hata kidogo....ni kibarua kizito sana kwangu mpaka nakuna kichwa sipati jibu nitaanzia wapi mpaka kweli watoto hawa wa Kitaliano wanielewe vizuri kwa kuimba kwa Kiswahili, pia bado nalaumiwa na marafiki kwanini sitafsiri habari hapa kwenye blog hii kwa kiitaliano, wao wanafuatilia wanapenda sana waelewe habari hizi, mimi sina mda wa kutafsiri kila habari na nawaambia lugha ya watu hii, ya kwangu tu inanishinda vizuri je hii lugha ngeni? hawanielewi kabisa, nalaumiwa kila siku, sasa tena na hili limejitokeza kazi kweli kweli!!!!. Yeye Isabella anasema wimbo wowote rahisi, sasa upi rahisi kweli??? Anasema hawa ni wanafunzi wake awapendao sana lazima nifanye hivyo...ametoka nao mbali wakiwa darasa la tatu na sasa wanamaliza darasa la tano, na kumaliza shule ya msingi, baada ya mda mfupi katikati ya mwezi huu tulio uanza watamaliza, maana wenzetu humaliza darasa la tano tu na humaliza mwaka wa shule katikati ya mwezi wa sita, huanza mwaka mwingine mwezi wa tisa. Sherehe ya kuwaaga itafanyika mwisho mwa mwezi huu...kweli nitaweza? na mimi wiki ijayo sipo ninasafiri kwa wiki nzima, nifanye nini? Leo niliweza kukutana na wafunzi hao, tukaongea mambo mengi sana, pia yalikuwa maswali mengi sana kuhusu Tanzania...nilicheka sana kwa maswali yao, ila wanaonekana wana akili za kushika mambo kwa haraka, na kesho kibarua kinaanza cha kuwafundisha wimbo huo..hata sijui nianzeje.
Isabella anapenda sana kiswahili na anajifunza kwa nguvu zote, pia matamshi yake ni mazuri sana utafikiri mswahili kabisa. Sasa ananiambia lazima waimbe kiswahili kwasababu ni lugha aipendayo sana, anasema nikitoroka nisipo fanya hivyo urafiki utaisha, kazi kwangu. Kama kuna mtu hapa anaweza kunisaidia kwa wimbo rahisi anao ujua...naomba anisaidie!

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Haya kaka Baraka sijui nimechelewa hapa nina wimbo nakumbuka tulikuwa tunaimba nilipokuwa darasa la mbili au tatu:- Una itwa MAUA MAZURI!
1.Maua mazuri yapendeza x2
Ukiyatazama utachekelea
Hakuna mmoja asiyeyapenda x2

2.Mtoto msafi apendeza x2
Ukimtazama utachekelea
Hakuna mmoja asiyempenda x2

3. Mtoto mtii apendeza x2
Ukimtazama utachekelea
Hakuna mmoja asiyempenda x2.

ray njau said...

Mama Sandra[mke wangu] ni mwalimu wa watoto na anazo nyimbo nyingi sana kwenye maktaba yake.Naamini ana nafasi nzuri ya kumsaidia.
-----------------------------------
**MOJA MBILI TATU,NNE TANO SITA,SABA NANE TISA,KUMI NAMALIZA.
----------------------------------

Baraka Chibiriti said...

Kweli dada Yasinta...umenipa wazo kuhusu huu wimbo maana ni rahisi. Ila mimi kuimba ni sifuri, nitajitahidi lakini.

Asante sana kwa wazo hilo.

Baraka Chibiriti said...

Mkuu Njau....mwambie mama watoto wako, nae achangie wazo lake. Nitashukuru sana...maana mawazo ya wengi..mara nyingi huwa ni faida sana.

WATEMBELEAJI