Thursday, June 3, 2010

KIBARUA CHANGU CHA KUFUNDISHA KIMEPAMBA MOTO SASA!

Kile kibarua changu cha kufundisha wimbo wa kiswahili...sasa kimepamba moto kweli kweli!!!! Wimbo umepatikana, ila ubize ndo usiambiwe kwasasa. Kila siku lazima niende huko na kurudi, km 100 kwenda na kurudi 50 kwa 50. Pia lazima mpaka nimalize kibarua changu rasmi kinachonipa chakula, la sivyo hakuna kula...ndipo nianze safari ya huko.

Baada ya kukuna kichwa kwa sana mpaka basi, sasa wimbo umepatikana, baada ya kuongea kwa simu na mama yangu akanikumbushia wimbo ambao nilikuwa naupenda sana tokea utotoni mwangu ndipo nikakumbuka, sasa tayari mafunzo yameanza...sasa sijui kama nitafanikiwa? Maana mimi mwenyewe mwanafunzi wa kuimba. Kuimba kwangu lilikuwa ni swala la mwisho kabisa mpaka sasa ni ziro kabisa, kupiga ngoma na vyombo mbalimbali vya muziki napenda sana...lakini sio kuimba. kazi kweli kweli...!!! Nikifanikiwa nitajitahidi kuchukua video, ili baada ya sherehe mshuhudie vichekesho vitakavyo kuwemo humo.

Pia asante sana Dada Yasinta kwa kunipa wazo na wimbo mzuri rahisi, ambao pia naufahamu vizuri...nitajitahidi kuutumia pia huo, kama ukinishinda huu nilio uanza kuufundisha leo.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nimefurahi kama umepata wimbo na tena tangu ulipokuwa mdogo umeuimba naamini utaweza tu. Nakutakia kila la kheri.Upendo daima

Baraka Chibiriti said...

Asante sana, nipo hapa naendelea kuwapa somo, naamini tutafanikiwa, maana nimeona wanaelewa kwa kasi.
Asante sana.

WATEMBELEAJI