Wednesday, June 2, 2010

KICHEKESHO CHA LEO..KAZI KWELI KWELI!!!!

Kuna ajali ilitokea maeneo ya Tazara. Baba mmoja mpita njia alisogea eneo la tukio, akamuona majeruhi mmoja amevunjika mguu, alikuwa akilia kwa machungu sana. Yule Baba alimuonea huruma sana, kwenda mbele kidogo akamkuta mtu mwingine kichwa kimeachana na mwili (amefariki). Yule Baba kuona hivyo akarudi kwa majeruhi wa kwanza...akamwambia; acha kudeka deka wewe!!! mwenzako amevunjika kichwa na halii, wewe muguu tu unalia nini???. Kazi kweli kweli....!!!!!

No comments:

WATEMBELEAJI