Saturday, June 12, 2010

WEEKEND NJEMA NA JUMAPILI NJEMA SANA KWENU NYOTE!

UJUMBE WA LEO;

Nitakushukuruje Bwana Mungu wangu, kwa mema mengi unayonijalia siku zote, kwani wewe ni mwingi wa rehema na rehema zako zapita kiasi.

Mema yote uliyotenda kwangu, umetenda kwa hakika. Na rehema ulizo nitendea, umetenda kwa hakika. Na chakula utulishacho ni kizuri kwa hakika, mbinguni unapoishi ni kuzuri kwa hakika. Twakushukuru kwa kutuumba, twakushukuru kwa kututunza, twakushukuru kwa kutuvisha, twakushukuru kwa kutupenda, kutupenda kwa hakika.

Sifa zako tutaziimba daima, wema wako tutauimba, huruma yako tutaimba, na fadhili zako tutaimba siku zote, tutaimba kwa hakika.

WATEMBELEAJI